+255 753 204 743 mkumbosj@gmail.com, facebook.com/mwlsamwelmkumbo

Thursday, April 25, 2013

MUNGU HUINUA.

Mungu huwapandisha watumishi wake kutoka Viwango hadi Viwango, na waweza kuona na kujifunza kutoka kwa watumishi kadhaa waliotutangulia na kupata uhakika katika haya ninayokuambia,. 
Wapo watumishi waliokuwa chini wakapandishwa na wapo waliokuwa juu wakashushwa halafu wakapandishwa tena kwa viwango na kasi ambayo Mungu alikuwa anataka. 
Wapo wengine walikuwa ni matajiri walipoanza kumtumikia Mungu wakapoteza vyote na kuwa Maskini na baadae wakarudi katika Utajiri wao na huku wakiendelea kumtumikia Mungu na kuwa Waaminifu kwa MUNGU. 

TUJIFUNZE KWA WALE WALIOTUTANGULIA

                                             Mwl: Christopher Mwakasege  


Si kwa watumishi walio wazee tu, lakini wapo na watumishi ambao ni vijana lakini wametoka katika hatua moja kwenda nyingine katika utumishi wao lakini kwa shida na dhiki lakini Mungu amewainua. na katika hayo twapata tumaini ya kuwa Huduma yako na utumishi wako na hali yako ya Kiroho bado ipo nafasi ya kuinuka na kupanda hatua na viwango vya juu Mtumishi wa MUNGU. 

                                       TWAWEZA KUJIFUNZA KWA WENGI. 


                                                 Mch: Abiud Misholi 

No comments:

Post a Comment

Home