+255 753 204 743 mkumbosj@gmail.com, facebook.com/mwlsamwelmkumbo
Shuhuda
Yesu apewe sifa.
Nilikuwa nakaribia kujifungua na muda umefika kabisa lakini hospitali wakawa wanasema watoto hawajageuka vizuri. nikatuma maombi yangu kupitia Mratibu wa Huduma (Kaka Japhet Mlomo) namshukuru Mungu nimejifungua vizuri na Mungu amekuwa mwema.
Atu, Makete-Njombe
Shalom,
Nilikuwa sina kazi, nilihudhuria Semina ya pale Yombo KKKT, nikatuma maombi yangu kwa kuwasiliana na Mratibu wa Huduma (Kaka Japhet Mlomo) namshukuru Mungu amejibu maombi yangu na sasa nimepata kazi.
KKKT-Yombo
Nashukuru kwa maombi yenu watumishi, maumivu ya tumbo hayapo tena na sasa nimeweza kwenda shuleni. Maumivu yalidumu kama dakika 20 baada ya maombi yalipotoweka hayakurudi tena na nikapata Nguvu na vichomi vikaisha kabisa. Mungu awabariki.
Stella, Dar es salaam
Ninamshukuru Mungu kwa mafundisho tunayopata kila siku asubuhi kutoka kwa Mwl. Mungu awabariki sana na nawaombea mzidi kututumia mafundisho haya. Nitakuwa nawatumia watu wasiopungua 30.
Emmanuel, Boko
Bwana asifiwe,
Mungu awabariki kwa mafundisho nimemwambia wakala anayenitumia haya asiache kunitumia kila siku, haswa huu mfululizo wa somo la Kuisoma Dira/ramani ya Mungu ili kufikia pamoja nae mahali uendako ni somo zuri ninaomba nitumiwe mpaka litakapoisha.
Dani, Arusha
Sitamani kuyakosa mafundisho yenu kila siku. Naomba pia msinisahau katika maombi yenu ya kila siku nimjue sana Mungu.
Mama Bujulu, Dar es salaam
Subscribe to:
Posts (Atom)
This comment has been removed by the author.
ReplyDeleteKweli tumeona mkono wa Bwana ukitenda makuu
ReplyDeleteKama si Mungu GKB na waseme sasa.
ReplyDelete