![]() |
Ev; Elisante Daniel |
Mungu ametuumbia kuwa na viungo tofauti mwilini vinavyofanya kazi tofauti ila kwa kutegemeana kati ya kiungo kimoja na kingine, lakini cha ajabu zaidi pamoja na kuwa kuna viungo hivyo; Mungu akaona ni vyema viongo hivi viwe na kiongozi wa kuwasikiliza na kuwaongoza.
Akaona ni vyema main controller(mtawala mkuu) na awe moyo.Kwa urahisi zaidi ni hivi: Rais wa nchi akitaka kuzuru mkoa fulani, mfano Tanga/Mtwara, kule mkoani kuna mkuu wa mkoa/jimbo ambaye Rais kabla hajaonana na wananchi (viungo) wa eneo hilo ni lazima kwanza angie kwa mkuu wa mkoa(moyo) .Mungu ni Rais; yeye akitaka kuja/kukutembelea,hawezi kuingia katika mkono,mguu/jicho ila anaingia na kubisha kwanza hodi mlangoni pa mtu, na mwenye nyumba(moyo) akimkaribisha yeye huingia na kukaa kwake, hata viungo vingine vyote vinapata taarifa ya kuwa kuna upako wa tofauti umetuzukia. Kwa maana nyingine ikiwa kidole ndicho cha kwanza kupokea upako;ule upako hauwezi kutembea kama radi au kusafiri kama miali ya jua kwenye viungo vingine;Kwanini? Jibu ni rahisi kidole sio kiongozi hivyo hawez i kutoa taarifa kwa wengine (viungo) kwa vile hana anuani zao,mwenye faili (documents) la wengine na kumbukumbu (records) za wengine ni moyo,na ndie kiongozi wa wengine.
Roho Mtakatifu, naomba unifundishe kuelewa kusudi lako moyoni mwangu, nilazima ufahamu kusudi la moyo wako kuwa ni kiongozi wa wengine na mwakilishi/balozi wa Mungu katika dunia hii tupitayo kama wasafiri. Yesu akitaka kuja kwako anatazama kama moyo wako ni balozi mwaminifu wa siri na nyaraka za Mungu au la hasha!,Rais wetu (Yesu) anasema”Tazama,nasimaa mlangoni ,nabisha ,mtu akisikia sauti yangu na kuufungua MLANGO(moyo) nitaingia kwake, nami nitakula pamoja nae, naye pamoja nami”(ufn 3:20).
Yesu ansema”........nasimama mlangoni nabisha.......”,hamaanishi mlango wa nyumba yako ya kifahari, ya udongo ama ya nyasi kama sio makuti, lahasha ila anamaanisha mlango wa moyo wako.Ngoja nikuonjeshe asali kidogo; Rushwa,ufisadi, ukabaji,ubakaji,mauaji ya kijambazi na mengineyo hayawezi kuiisha katika mkoa/nchi ikiwa mkuu/kiongozi wa eneo hilo hana msimamo wa uadilifu na malezi mazuri katika kundi lake na msimamo wa uadilifu wa kiongozi huyu hutokana na hofu ya Mungu kukaa ndani yake , Vivyo hivyo viungo vya mwili havitaacha kujiingiza katika ulevi,uzinzi,ukahaba,ulafi,ufitina,uongo.......kama moyo hauna msimamo unaotokana na utajiri wa maadili na maonyo ya hofu ya Yesu ndani yake. Hofu ya Mungu haiwezi kuingia ndani ya mtu ikiwa mlango wa moyo wake umefungwa; ni lazima ufunguliwe pale Yesu anaposimama kwako na kubisha hodi.
Sijawahi kuona kwenye Biblia sehemu imeandikwa “Heri wenye macho safi au miguu safi maana hao watamwona Mungu” bali nimeliona hili tu “Heri wenye MOYO safi maana hao watamwona Mungu”.Math 5:8
Ibada ya mtu na Mungu inakuwa ndani ya MOYO wake mwenyewe,na IMANI pia injengwa ndani ya MOYO,ndo maana Biblia imeendika KWA MOYO MTU HUAMINI HATA AKAHESABIWA HAKI..........Rum 10:9-10
SIRI YA WOKOVU ILIYOJIFICHA NI KUMPA MUNGU NAFASI MOYONI
No comments:
Post a Comment