Huduma ya NURU ni huduma isiyofungamana na dhehebu lolote au tunaweza kusema ni Huduma inayohusisha watu wa Madhehebu yote wanaokiri Wokovu. Ikiwa na msingi wake tangu mwaka 2008. Huduma ya NURU ina Timu yenye watu 16 ndani yake ikiwa na Viongozi Watano katika kusimamia Utekelezaji wa Maono na Mipango ya huduma. Ni Huduma inayoendeshwa kwa mtindo wa Mafundisho ya Neno la MUNGU (Huduma ya Ualimu)
Kwa kuwa
Mungu, aliyesema, Nuru
itang'aa toka gizani, ndiye
aliyeng'aa mioyoni mwetu,
atupe nuru ya elimu ya utukufu wa Mungu katika uso wa
Yesu Kristo (2
Wakorintho 4:6)
Kwa
ujumla wake na
katika mambo au
Huduma zote zinazofanywa
na NURU katika kutenda
kazi ya Kueneza
Ufalme wa MUNGU,
jambo la msingi
tuombalo kwa BWANA kwa
unyenyekevu na ambalo
tunatamani MUNGU atutendee
sisi na wewe pia kwa kuwa ni muhimu ni hili;
…….ATUPE NURU
YA ELIMU YA
UTUKUFU WA MUNGU
KATIKA
USO
WA YESU KRISTO..
Na hii ndio kazi ya Mafundisho ya Neno
la MUNGU yanapopita mahali popote, na ndio
kazi kubwa ya
Huduma ya Ualimu
ndani ya Kanisa
nalo ndilo tunalihitaji pia kutoka kwa MUNGU atusaidie
kufundisha mafundisho yafaayo kuwapa watu Elimu ya MUNGU. Naam na iwe hivyo kwa
Huduma zote za Ualimu.
Tuaminivyo:
Ø
Kama
Huduma Tunaamini katika MUNGU Baba, Mwana na Roho Mtakatifu (UTATU MTAKATIFU)
Ø Tunaamini ya kwamba YESU ALIKUFA MSALABANI NA SIKU YA TATU ALIFUFUKA KUTOKA KWA WAFU NA YU HAI MILELE na ya kwamba ATATUFUFUA nasi siku ya mwisho.
Ø Tunaamini WOKOVU WA MWANADAMU unapatikana kwa KIFO CHA YESU MSALABANI.
Ø Tunaamini katika Biblia (Maandiko Matakatifu) yenye Vitabu 66 kama msingi wa Mafundisho yetu.
Ø Tunaamini WATU TULIOOKOKA tumepewa Jukumu la kuwaeleza watu wote na Ulimwenguni Kote habari Njema za Msamaha wa Dhambi kwa Kumwamini BWANA YESU KRISTO.
Huduma
tunazofanya:
Huduma ya NURU hufanya huduma
mbalimbali ambazo lengo lake ni kufikisha mafundisho ya Neno la MUNGU kwa watu
wote wenye uhitaji wa mafundisho. Katika kutenda hilo Huduma ya NURU hufanya
kazi zifuatazo;
SEMINA: hujumuisha semina za kuandaliwa na Makanisa na makundi mbalimbali na zile za kuandaa wenyewe (yaani Huduma ya NURU)
MAKONGAMANO: Ni mafundisho maalumu kwa makundi maalumu, kama vile wafanyabiashara, wanafunzi, viongozi n.k
MAFUNDISHO KWA NJIA YA MTANDAO: Pia tunafanya mafundisho kwa njia ya mtandao, hapa hujumuisha mitandao ya Kijamii, tovuti na Barua pepe na pia kwa simu za mikononi kwa njia ya Whatsap na sms.
MAFUNDISHO
KWA VIDEO NA AUDIO:
Pia yapo mafundisho kwa njia ya video na audio (kusikiliza) ili kwa wale ambao
hawajawahi kuhudhuria Semina zetu au makongamano basi wanaweza kufanikiwa
kupata mafundisho hayo kwa njia hizo.
No comments:
Post a Comment