GOMBO LA WIKI
Na: Samwel Mkumbo
Sehemu
ya 1.
“HUZUNI YA JINSI YA MUNGU”
Katika
GOMBO LA WIKI hii ninakufundisha kuhusu “HUZUNI YA JINSI YA MUNGU”, na hii ni kutokana na swali
nililoulizwa na ndugu mmoja kutokana na kitabu cha 2
Wakorintho 7:10, umeandikwa hivi;
“Maana huzuni iliyo kwa jinsi ya
Mungu hufanya toba liletalo wokovu lisilo na majuto; bali huzuni ya dunia
hufanya mauti.”
KARIBU!!
Inawezekana si Neno geni kwako kusikia “HUZUNI YA JINSI YA MUNGU” na inawezekana kwako ni geni pia jambo hili lakini sote tulete mawazo yetu hapa! Weka moyo wako kwenye Utulivu ili nikufundishe na Roho Mtakatifu aseme nawe juu ya hili KWA JINA LA YESU, Neno Hili Likawe Na Nguvu Na Lenye Kuponya KWA JINA LA YESU Na Kuleta Hekima Ndani Yako KWA JINA LA YESU. Aaamen
Ili
kuweza kuyatenda mapenzi ya Mungu ni muhimu kuyajua na ili kuyajua mapenzi yake
basi yanapatikana kwa kulijua Neno lake, naam!, Neno ndilo limebeba maelekezo
ya Mungu, sasa basi moja ya jambo Mungu ameliweka bayana ni pale mwanadamu
anapokosea ni KUTUBU na KUREJEA, naam, ni “Kutubu na Kurejea”.
37Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo
yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, Tutendeje, ndugu zetu? 38 Petro
akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate
ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu ( Matendo 2:37-38)
Kabla
sijaendelea kukueleza mengi labda nikupe maelezo haya kwanza, TOBA ni “Tokeo”
yanayoleta “Matokeo”, naam! Ni sahihi, na nirudie tena kukazia hapo Toba ni
TOKEO LINALOLETA MATOKEO. Na hii ni kwa sababu kabla “Toba” haijafanyika kuna
mambo” Yanayootangulia” na baada yake kuna mambo “Yanayofuata” ndio maana ni
kasema kuwa……. Toba ni Tokeo linaloleta Matokeo……., na hiyo ni muhimu kuijua
sana sana maana ..,,…,..tunaweza tusithamini toba kwa maana hatujui matokeo
yake, lakini pia ,,..,,..,,tunaweza tusithamini toba kwa kuwa hatujui
inasababishwa na nini……… lakini pia tunaweza kuifanya kwa mazoea kwa kuwa
hatujui inatokana na nini na itazaa nini.
Lakini
katika Somo hili nitasimama kwenye upande wa kukufundisha KUTUBU kama TOKEO
lililotokea kutokana na mambo kadhaa.
Matendo 2:37 inasema hivi;
37Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo
yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, Tutendeje, ndugu zetu?
Katika
mstari huo tunaona jinsi gani unaweza kuona kwamba Kutubu ni Tokeo linalokuja
baada ya mambo kadhaa kutokea na mojawapo tumeliona hapo juu, biblia inanena
hivi……37Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao.,..,…”
MAMBO
YANAYOTANGULIA ILI TUPATE KUTUBU
Kuna
mambo kadhaa yanayotangulia ili kutupa Nguvu na Wito wa kutubu na haya ni
muhimu kuyafahamu maana kwa kutojua haya wengine wameishia kutojua nini cha
kufanya yanapotokea katika maisha yao ya kila siku, na wengine yamewatokea
wakaishia kwenye hayo pasi kwenda hatua iliyo ya muhimu ambayo ni “Kutubu”
Kutambua
dhambi /kosa
Hili
ndilo jambo la kwanza aambalo huleta matokeo ya kutubu juu ya jambo lolote
lile, nah ii inatupa kuelewa zaidi pale ninapikwambia Kutubu ni Tokeo, na moja
ya sababu ya tokeo hilo ni “Kutambua Kosa” ambalo mtu au watu wanakuwa nalo.
Kwa habari ya Mfalme Daudi katika Zaburi 51:3 tunasoma maneno haya:
“Maana
nimejua mimi makosa yangu ,na dhambi yangu i mbele yangu daima ".
Daudi
anasema kwa Mungu kuwa jambo linalompa Kutubu au jambo lilimpelekea kwenda kwa
Mungu kuomba msamaha analisema hivi “…. Maana NIMEJUA mimi MAKOSA yangu……”
Watu
wengi tumekuwa hatupati msamaha wa dhambi kwakuwa hatuko tayari “Kutubu” na hii
ni kwasababu hatuna utayari na hatutaki “Kutambua” dhambi zetu.
Kosa
letu ni kuwa tunarahisisha dhambi na kufanya kuwa ni jambo la kawaida, na mara
nyingi kwa mawazo na maneno yetu au hata matendo yetu tumehalalisha haramu na
kuharamisha halali NI MBAYA.
Ni
muhimu kuelewa kwamba unapojikuta “Umetambua” ya kuwa unalo kosa mbele za Mungu
ni nafasi yako ya kwenda Kutubu na pia ukiona unapata hamu ya Kutubu basi ujue
ndani kama nje bado hujaona jua tu roho yako imetambua kuna kosa mahali na ndio
maana unapata hamu ya kutubu usianze kufikiri-fikiri anza Kutubu na utaona
jinsi Mungu anavyolifunua hilo ulilolitambua rohoni.
Kujutia
dhambi.
Ili
mtu aweze kujutia dhambi ni lazima kuwepo na mguso wa ndani ya moyo (nafsi
yake), lakini hii si hatua ya mwisho, maana wengi wanapotoka hatua ya kwanza
(Kutambua Kosa) huwa wanaishia kwenye hii hatua ya pili ya “Kujutia” lile
alilolitambua kuwa ni kosa ndani yake na huwa wanaishia hapo,
Luka
15:17 utakuta maneno haya:-
Alipozingatia
moyo mwake alisema ……………….. mwana
mpotevu hakuwa na chakufanya baada ya kutambua dhambu yake ila kwanza kujutia
moyoni. NAHATUWEZI
KUJUTIA DHAMBI BILA YAKUITAMBUA DHAMBI.
Itaendelea,……..
Ni somo zuri na MUHIMU sana
ReplyDeleteAsante sana!!