JIANDAE KURUDI NYUMBANI (SEHEMU YA 1)
Mwl; Samwel Mkumbo
Utangulizi:
Maana hapa hatuna mji udumuo, bali twautafuta ule ujao. (Waebrania 13:14)
Mtu huweza kutoka asubuhi kwenda katika shughuli mbalimbali wengine huenda mashambani wengine maofisini na wengine kwenye shughuli za aina nyingine, biashara lakini ifikapo jioni au usiku HURUDI NYUMBANI, inawezekana kama ni watoto au ni wazazi waliachana asubuhi wengine wakienda kazini wengine shuleni lakini jioni WATARUDI NYUMBANI.
Mtu anapotoka mji mmoja na kwenda mji mwingine kwa ajili ya kuishi huko aidha kwa sababu za kikazi au hata biashara, akafanikiwa na akaanzisha maisha huko akawa na familia huko na akajenga na makazi yake huko, lakini siku akifariki mara nyingi wengi HURUDISHWA kuzikwa NYUMBANI.
Katika kitabu hiki ambacho kitakusaidia kukueleza mambo kadhaa juu ya wokovu ulioupokea katika maisha yako, utajifunza mambo mengi na ni maombi yetu ya kwamba kitabu hiki kiwe msaada mkubwa sana kwako.
Mambo utakayojifunza:
Sura ya Kwanza: katika sura ya kwanza utajifunza namna ambavyo dunia hii si mahali pa kupategemea na ya kwamba si mahali pa kudumu, na pia utajua kama dunia si mahali pa kupategemea je hatma yako ni nini, na ni nini mwisho wa maisha yako.
Sura ya Pili: itakusaidia kujua ni nini unachotakiwa kufanya kama dunia si mahali pa kudumu ili uweze kufika unakotakiwa kwenda, utajifunza kuwa unahitaji sana maandalizi ya kuelekea mahali unapotakiwa kwenda.
Sura ya Tatu: mambo ya msingi ikiwa ni mwendelezo wa sura ya pili ni kujua ya kwamba unakokwenda hutakiwi kwenda mikono mitupu, kuna mambo unayotakiwa kuyabeba, hivyo kwanza utajikuta kuna maswali unatakiwa kuyajibu ya ulichobeba kwanza na kisha utajua ni nini unatakiwa kubeba.
Sura ya Nne: sura hii itakuelekeza mambo ambayo ni muhimu uyafahamu katika safari hii, mambo yatakayotokea njiani, mambo ambayo yanapotokea usishangae, lakini pia utapata tumaini kwa kujua ya kwamba hauko peke yako.
Nimalizie utangulizi huu kwa kusema JIANDAE KURUDI NYUMBANI.
GOMBO LA WIKI
Na: Samwel Mkumbo
“HUZUNI YA JINSI YA MUNGU”
Katika wiki hii tunaendelea na mtiririko wa kujifunza somo linaloitwa “HUZUNI YA JINSI YA MUNGU”, na wiki iliyopita tulijifunza mambo kadhaa, na mstari wetu mkuu tunaoutumia katika Somo hili ni ule wa 2 Wakorintho 7:10 na katika huo tutajifunza mengi zaidi……..
MASOMO YALIYOPITA
No comments:
Post a Comment