Na:
Mwl. Samwel Mkumbo
KANISA ni Nafsi za watu zilizounganishwa kwa kunia mamoja katika Imani yao na hiyo Imani wameijenga katika msingi wa YESU KRISTO, hivyo kanisa bila ya nafsi zilizokubaliana za watu wengi wa aina mbalimbali si kanisa maana ili wawe kanisa lazima nafsi zao ziungane kwa kunia mamoja na kuwa na Imani moja ambayo hiyo Imani ndiyo inatengeneza nia moja.
Uhai wa kitu chochote kile
unategemea namna au jinsi mwenye huo uhai au aliyekabidhiwa dhamana yuko katika
hali gani, unaweza kulaumu juu ya uharibifu wa jambo au mambo Fulani lakini
kabla ya kulaumu angalia kwanza yeye aliyeharibu au aliyekabidhiwa mikononi
mwake yuko katika hali gani.
MATENDO
20:28 inasema hivi;
Jitunzeni
nafsi zenu, na lile kundi lote nalo, ambalo Roho Mtakatifu amewaweka ninyi kuwa
waangalizi ndani yake, mpate kulilisha kanisa lake Mungu, alilolinunua kwa damu
yake mwenyewe.
Sasa kabla sijaendelea Zaidi nataka niseme jambo la msingi sana hapa, kichwa cha Somo letu kinatuhitaji tuwe na ufahamu wa kuhakikisha kwamba kila tunachokiongea katika somo hili ni mambo makubwa mawili, NAFSI YAKO NA KANISA LAKO. Wewe ni nafsi moja katika kanisa, Je unayo kazi gani wewe kama Nafsi?
Unaweza usijue wala
usiliangalie kwa uzito, lakini inapasa kuelewa tafsiri hii;
KANISA
ni
Nafsi za watu zilizounganishwa kwa kunia mamoja katika Imani yao na hiyo Imani
wameijenga katika msingi wa YESU KRISTO, hivyo kanisa bila ya nafsi
zilizokubaliana za watu wengi wa aina mbalimbali si kanisa maana ili wawe
kanisa lazima nafsi zao ziungane kwa kunia mamoja na kuwa na Imani moja ambayo
hiyo Imani ndiyo inatengeneza nia moja.
TAZAMA
NAMI:
Ili kanisa liwe na Nguvu na
likae katika mstari unaotakiwa ni lazima nafsi za watu ndani ya Kanisa ziwe
ziko salama kabisa, yaani ziwe zimetunzwa katika hali ambayo uhakika wa kundi
kuishi kwa Amani utakuwepo kwa uhakika.
Labda tuunganishe vipande
viwili vya huo mstari wetu wa msingi ili uone jambo la msingi kidogo….. Jitunzeni nafsi zenu,,.,.. mpate kulilisha
kanisa lake Mungu,.,.,..
Mfano wa Mtumwa Mwaminifu
Bwana
akasema, Ni nani, basi, aliye wakili mwaminifu, mwenye busara, ambaye bwana
wake atamweka juu ya utumishi wake wote, awape watu posho kwa wakati wake? Heri
mtumwa yule, ambaye bwana wake ajapo atamkuta anafanya hivyo. Kweli nawaambia,
atamweka juu ya vitu vyake vyote. Lakini, mtumwa yule akisema moyoni mwake,
Bwana wangu anakawia kuja, akaanza kuwapiga wajoli wake, wanaume kwa wanawake,
akila na kunywa na kulewa; bwana wake mtumwa huyo atakuja siku asiyodhani na
saa asiyojua, atamkata vipande viwili, na kumwekea fungu lake pamoja na
wasioamini (LUKA 12:42-46)
Sasa hapo ninataka
nikufundishe jambo ambalo kimsingi ambalo halipo kwenye Mistari hiyo hapo juu,
na lenyewe ni juu ya adhabu aliyopewa huyo wakili. Ona mtari huu;,..,.. akaanza kuwapiga wajoli wake,
wanaume kwa wanawake, AKILA NA KUNYWA NA KULEWA;,.,….
Maana suala sio kusema bwana
wake anachelewa ila baada kuona bwana wake anachelewa alifanya nini? Na wala
sio kuwapiga watumwa ila baada ya kuwapiga watumwa alifanya nini? Yeye
alichokifanya ni KULA NA KUNYWA NA
KULEWA,..,..
Biblia inaposema yeye
ALIKULA NA KUNYWA NA KULEWA, maana yake aliacha kufanya alichotakiwa kufanya
lakini pia aliiharibu nafsi yake kwa MVINYO yaani kwa Ulevi. Maana suala si
kula na kunywa kwa sababu hayo ni mahitaji ya mwili wa kila mtu, lakini suala
ni KULEWA na biblia inasema KILEO HUDHIHAKI,. Na pia HUPOTOA HUKUMU ZA HAKI.
MAANDIKO KADHAA:
1
YOHANA 5:20-21 inasema hivi;
Nasi
twajua kwamba Mwana wa Mungu amekwisha kuja, naye ametupa akili kwamba tumjue
yeye aliye wa kweli, nasi tumo ndani yake yeye aliye wa kweli, yaani, ndani ya
Mwana wake Yesu Kristo. Huyu ndiye Mungu wa kweli, na uzima wa milele. Watoto
wadogo, jilindeni nafsi zenu na sanamu.
Sasa ninatamani tuangalie
jambo zuri kidogo katika mstari huo hapo, ya kwamba msisitizo wa maneno ya
mtume Yohana juu ya hayo aliyoandika haupo kwenye kutaka kuwaeleza habari ya
Kuthibitisha kuwa YESU AMEKWISHAKUJA, wala pia si juu ya Habari ya kutaka kuwaeleza
kuwa WAO WALIOAMINI WAKO NDANI YA YESU AMBAYE NI KWELI NA MUNGU WA KWELI,
lakini hayo yote aliyasema ili kuipa nguvu sentensi yake ya mwisho ya kuwaambia
JILINDENI NAFSI ZENU SANAMU.
TAZAMA
NAMI:
Sasa tukianza kuangalia
maneno ya Yohana kabla hajatoa msisitizo wa kuilinda nafsi zetu dhidi ya
Sanamu, maneno yaliyotangulia kuna mahali yanatuelekeza;
Nasi
twajua kwamba Mwana wa Mungu amekwisha kuja, naye ametupa akili kwamba tumjue
yeye aliye wa kweli, nasi tumo ndani yake yeye aliye wa kweli, yaani, ndani ya
Mwana wake Yesu Kristo. Huyu ndiye Mungu wa kweli, na uzima wa milele………
Sasa kwenye huo mstari
nataka kwanza Ninyofoke na lile neno Nasi
TWAJUA.,.. ikiwa na maana kwamba hayo yatakayofuata au atakayoyasema
YANATOKA KWENYE UFAHAMU au ni UJUZI alionao juu ya Mungu, na Yesu Kristo mwana
wake wa pekee.
Kwa hiyo Yohana anaposema
kule mwishoni ya kwamba JILINDENI NAFSI ZENU NA SANAMU, maana yake JILINDENI
NAFSI ZENU NA UJUZI AMBAO HAUTAELEZA JUU YA HAYO ALIYOELEZA, kila KUJUA
kusikokuonesha wewe ni nani mbele za MUNGU ni wa kujilinda nao, ujuzi
usiokuwambia habari ya dhambi zako, ni wa Kujilinda nao, Ujuzi usiokuwambia ya
kwamba dhambi zako zinaweza kusamehewa kwa Damu ya YESU iliyomwagika pale
Msalabani huo Ujuzi ni wa Kujitenga nao, Ujuzi wowote usiokwambia kwamba
unahitaji utakatifu kwa kiwango cha juu, na uache dhambi zako, uache kukaa na
wenye dhambi kama si suala la kuwahubiria injili, ujuzi usiokwambia usikae
mahali wanauza pombe, usiangalie dansi, usiangalie watu watendao mambo ya aibu,
usiweke chaneli mbaya zinazoweza kuharibu watoto ujuzi usikwambia hivyo ni wa
KUJITENGA NAO.
TAZAMA
NAMI:
Ujuzi wowote unaokuja kwako
unakuja kwa malengo makubwa yafuatayo, na ambayo ni lazima mtu ujiulize kwa
undani sana ili upate kuona ni nini iko nyuma yake…,..,.
Kupima
namna unavyojua au ujuzi wako au
ufahamu
wako juu ya jambo Fulani.
Mwanzo
3:1
inasema hivi:
Basi
nyoka alikuwa mwerevu kuliko wanyama wote wa mwitu aliowafanya Bwana Mungu.
Akamwambia mwanamke, Ati! Hivi ndivyo alivyosema Mungu, Msile matunda ya miti
yote ya bustani?
Ukitazama msingi wa hilo
swali kwa undani utagundua shetani alikuwa na majibu ya swali alilouliza au
alikuwa hana uhakika na majibu aliyokuwa nayo juu ya swali alilouliza au
alikuwa anataka kulinganisha majibu yake na ya Hawa kuhusu kile anachofahamu
juu ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya. Kwa hiyo ALIKUWA ANAPIMA HAWA ANAJUA
NINI JUU YA MTI WA UJUZI WA MEMA NA MABAYA.
Basi
Yesu akasema, Bado kitambo kidogo nipo pamoja nanyi; kisha naenda zangu kwake
yeye aliyenipeleka. Mtanitafuta wala hamtaniona; nami nilipo ninyi hamwezi
kuja. Basi Wayahudi wakasemezana, Huyu atakwenda wapi hata sisi tusimwone? Ati!
Atakwenda kwa Utawanyiko wa Wayunani, na kuwafundisha Wayunani? (YOHANA
7:33-35)
Ukitazama namna swali la
Wayahudi limekaa katika mtindo ambao wanajaribu kupima ufahamu wa YESU kwa
kuangalia ufahamu walionao wao, yaani ya kwamba YESU ana uhakika na hicho
anachokisema hapo.
Itaendelea... DOWNLOAD HERE
No comments:
Post a Comment