“BWANA ASEMA HIVI, TAZAMA, NAWEKA JIWE KATIKA SAYUNI, LIWE MSINGI, JIWE
LILILOJARIBIWA, JIWE LA PEMBENI LENYE THAMANI, MSINGI ULIO IMARA; YEYE AAMINIYE
HATAFANYA HARAKA.” ISAYA 28:16
Kuna mambo ya msingi yanayoendana sana na maandalizi yako ya
mtihani wa kumalizia mwaka wako wa masomo! Na ikiwa Yesu alisema sisi si wa
ulimwengu huu (Yoh 17:14) basi hata jinsi ya maandalzi na technique zetu katika
maandalizi YASITEGEE SANA kwa jinsi ya hao wa ulimwengu huu wafanyavyo!
Isay 28:16 ina maneno yenye maana kubwa sana ukiyafahamu
hasa kipindi hiki cha maandalizi yako ya UE (UNIVERSITY EXAM), labda tuu
nianze:
Anavyosema “NAWEKA
JIWE KATIKA SAYUNI, LIWE MSINGI” Unapata picha gani?
Kwanini anasema analiweka Sayuni na sio sehemu nyingine? Afu
si tu kwamba anaweka jiwe, lakini jiwe hilo liwe msingi… haya ni maswali
niliojiuliza kabla sijafahamu kitu halisi
Neno Sayuni kwenye Biblia limetumika sana kama mahali
panapohitajika wokovu au panapotokea wokovu
mfano Zab 53:6 “Laiti wokovu wa
Israeli utoke katika Sayuni” angalia pia( Zab 20:1-2, Mika 4:2, Isaya 28:16)
Hivyo nikija kwenye mazingira ya sasa
Ni ukweli usiofichika kuwa upo
Sayuni; na Mungu anasema anaweka jiwe la msingi hapo Sayuni.
Hili jiwe la
msingi ni nini?
Ili tuwezekujua hili jiwe la msingi ni nini, angalia sifa
zake, Isay 28:16 “LILIJARIBIWA,JIWE LA
PEMBENI,LENYE THAMANI,MSINGI IMARA” Always mawe yanayotumika kujenga msingi
hayafanani na mawe ya ujenzi wa nyumba kwa uimara. Mara nyingi msingi unahitaji
mawe au matofali yaliyo bora zaidi na ukijaribu kuchunguza baadhi ya nyumba, msingi uliwagharimu sana kupita
ujenzi wa juu ya msingi. Kwa picha hiyo
NENO LA MUNGU ( angalia Zab 12:6) limewekwa katika picha ya JIWE lakini pia kwa wakati huo Mungu alikuwa anamwongelea
YESU, Lakini kuna mahali Yesu anaongeleka kama NENO (Yohan 1:1-2,14).
Hivyo JIWE ni NENO LA MUNGU, Na Mungu anasema analiweka Sayuni yaani mahali
unapohitaji WOKOVU au unahitaji MSAADA. Embu soma hii mistari afu itafakari:
“HULITUMA NENO LAKE, HUWAPONYA, HUWATOA KATIKA MAANGAMIZO YAO” ZABURI
107:20
“KUMBUKENI MAMBO YA ZAMANI ZA KALE; MAANA MIMI NI MUNGU WALA HAPANA
MWINGINE……….NITANGAZAYE MWISHO TANGU MWANZO” ISAYA 46:9-10
Hiki ni Kipindi ambacho Mungu huweka NENO lake kwenye
mazingira unayopitia, Mungu ni kama MPAZI anavyoongeleka kwenye (Luka 8:4-8) Neno
hilo ni la kukupa tumaini, NENO lake anataka liwe MSINGI maana yake liwe ndo
msukumo mkubwa kwako wa TUMAINI LA KUFAULU Kujiandaa kwako kwa kusoma, ufanyaji
wako wa mitihani, kusuburia kwako matokea na mengine mengi yanayohitajika
kipindi hiki cha maandalizi VIJENGWE JUU YA MSINGI HUO.
Unachotakiwa kufanya TAFAKARI SANA hilo neno maana najua
unalo, unavyozidi kutafakari ndivyo unavyozidi KUSIKIA na UNAVYOZIDI KUSIKIA
kwa kutafakari ndivyo unavyoongezeka IMANI. Maana yake “IMANI
HUJA KWA KUSIKIA, NA KUSIKIA HUJA KWA NENO LA MUNGU”
Sasa mstari wa mwisho “yeye
aaminiye hatafanya haraka” Isaya 28:16 huu mstari ulinishangaza na
nitakuonesha vitu viwili vilivyonishamgaza,
- Angalia “HATAFANYA HARAKA” anamaanisha nini? Ukisoma kwenye amplified Bible ameandika “ WILL NOT PANIC ”
- Angalia neno “HATAFANYA HARAKA” Hili neno “HATA-” linaweka kipimo cha kiwango cha IMANI inayohitajika, maana yake UKIPANIC ujuwe huna hii imani inayoongelewa hapo.
KUPANIC maana yake huamini kuwa itawezekana, na pia
humwamini aliyekwambia kuwa atakusaidia hivyo KUPANIC ni DHAMBI, Embu soma huu
mstari vizuri
“naye afanyaye haraka
kwa miguu hutenda dhambi” MITHALI 19:2b
“the one who act hastily
sin” - from Holman Christian Bible
“to be overhasty is to sin and to miss the mark (or goal)” – from
Amplified bible
Mungu anakitu anataka kufanya kipindi hiki kwenye masomo
yako na ndio maana ameleta ujumbe huu
kwako, hivyo usome tena na tena na tena.
Nakutakia mtihani
mwema na mafanikio tele unapoendelea na maandalizi yako ya UE.
BY Mwl JOSHUA SHOO
No comments:
Post a Comment