Divai
MPYA!!!!!!!!!!
Ni wazi kabisa ya kuwa katika mabadiliko ya nyakati
hasa za ulimwengu yapo mambo mengi sana ambayo tunahitaji kujifunza sana huku
tukitazama namna ya kuendana na mabadiliko hayo.
Hakuna
mtu atiaye kiraka cha nguo mpya katika vazi kuukuu; maana kile kilichotiwa
huondoa kipande cha lile vazi, na pale palipotatuka huzidi. Wala watu hawatii
divai mpya katika viriba vikuukuu; na kama wakitia, vile viriba hupasuka, divai
ikamwagika, na viriba vikaharibika; bali hutia divai mpya katika viriba vipya,
vikahifadhika vyote…,..,.. (Math 9:16-17)
Japokuwa watu wamekuwa wakitumia mstari huu kujaribu
kuhalalisha mabadiliko HASI yanayoingia katika kanisa na hata kufikia kuona
Ndio mwelekeo Halali wa kanisa hasa kwa vijana na kuona kuwa ni “Divai mpya” na wao ni “viriba vipya”(vijana).
Lakini hiyo haikuwa maana ya Yesu katika mfano huo
maana alichokuwa anakionesha ni namnagani walivyotakiwa kuenenda hao mafarisayo
wanaotii sheria na wale wanaomtii Kristo yaani wale waaminio wokovu huja kwa
neema ya Kristo. Tazama hapa;
Wakati
ule wanafunzi wake Yohana wakamwendea, wakasema, Kwa nini sisi na Mafarisayo
twafunga, bali, bali wanafunzi wako hawafungi?......(Math 9:14)
Tunachoweza kuona hapo ni juu ya suala la wanafunzi
wa Yohana kutaka kufananisha nyakati za Yohana na Yesu pasi kujua mabadiliko ya
nyakati na YESU aliwapa mfano ambao ulikuwa ni jawabu la ndani ya mioyo na
fumbo la Imani,.
Naam, kinachotazamwa hapo ni namna ambavyo wanafunzi
wa Yohana hawakujua hali iliyopo ndani ya Ukristo, naam hata yale mafundisho
hayakuwa katika namna ambavyo wangeelewa kwa haraka kwa jinsi ya kawaida, kwao
haikuwa rahisi kujibadili na kujua Neema iliyopo katika Kristo, bali walitaka
kuona ni kwa namna gani wanaweza kuwasaidia wanafunzi wa Yesu ili nao wapate
kushika mapokeo.
Lakini
Tito aliyekuwa pamoja name, naye ni Myunani, hakulazimishwa kutahiriwa. Bali
kwa ajili ya ndugu za uongo walioingizwa kwa siri ili kuupeleleza uhuru wetu
tulionao katika Kristo Yesu, ili watutie utumwani..,,..,,..
(Wagalatia 2:3-4)
Katika kutazama hapo utagundua ya kuwa hao wanafunzi
wa Yohana walichunguza uhuru wa wanafunzi walionao katika Kristo ndiposa wakaja
na hoja au ushauri kwao, lakini jawabu la Yesu linatupa kuona ni kwa jinsi gani
ilivyo vigumu kwa watu walio katika mlengo Fulani wa imani au wanaoshikilia
msimamo Fulani wa Imani inavyokuwa ni vigumu kuishi katika mfumo mwingine wa
imani.
Na kama ukisoma vizuri mistari ile ya Mathayo, ule
mtari wa 16 unaendana na Yohana 1:17 unaosema hivi; …. Kwa kuwa torati ilitolewa kwa
mkono wa Musa; neema na kweli zilikuja kwa mkono wa Yesu Kristo…..
Ndiposa waweza kuona hao walioishi kwa Sheria basi
watahukumiwa kwa sheria na hao walioishi kwa Neema naam nao watahukumiwa kwa
Neema.
Basi Divai
MPYA huwekwa katikaviriba vipya maana ni yenye nguvu tena uhitaji mahali
penye uwezo wa kutunza maana viriba vya kale vimechoka kwa kujaza divai
iliyoisha ukali wake kwa kukaa muda mrefu na kupoteza ladha yake tena huwa ni
kama kuweka kiraka cha nguo mpya katika vazi kuukuu maana hata rangi na mng’ao wake
hutofautiana sana na hilo ndilo alilokuwa analisemaBwanaYesu hasa katika kujua
nafasi ya jambo jipya na ndio maana sisi hatuwezi kumbeba Kristo katika miili
yetu hii iliyochoka na kuchakaa hasa miili yenye taabu na majuto.
Tunahitaji kubadilishwa kwanza na kuwa watu wapya
kabisa.
No comments:
Post a Comment