Kristo asifiwe. Ninamshukuru
sana Mungu kwa ajili yako wewe msomaji wa ujumbe huu kwa nafasi ambayo
Mungu anaendelea kukupa Maishani Mwako. Zab 118:24 (Siku hii ndiyo
aliyoifanya Bwana nasi tutaifurahia.) Furaha ni mwonekano
unaoanzia ndani ya mtu hata kuonekana nje kutokana na vile aonavyo ndani
yake. Hivyo furaha ni jambo lililo chini ya uamuzi wako. Biblia inasema
kila siku aliyoifanya Bwana ni ya furaha.Maana yake unapoamka
asubuhi na kukiri maneno haya haijalishi utakutana na nini lakini Mungu
ataitunza furaha yako. Shetani anachotamani ni wewe usiwe na
furaha maishani mwako. Asante Bwana Yesu uliyetupa siku mzuri ili
tufurahi. Furaha inakuja kwa mambo makuu matatu.
1. Ukiri wa kinywa
chako kwamba utakuwa na furaha.
2. Imani kwa Mungu wako akupaye furaha.
3.Kuikubali siku hii kwamba imetoka kwa Bwana.
Ukifanya hivyo haijalishi kitu gani kimetokea kwako, kizuri au kibaya Mungu atashughulika. Utakuwa huru kila utakapokuwa. Yohana 8:36. Basi mwana akiwaweka huru mtakuwa huru kweli
No comments:
Post a Comment