Mwj: Emmanuel Molell M |
MASWALI UNAYOJIULIZA YAMEKWAMISHA MAJIBU YA MAOMBI YAKO
Nafurahi kujumuika nawe mtu wa Mungu ktk ujumbe huu kwa njia ya mtandao
Nafurahi kujumuika nawe mtu wa Mungu ktk ujumbe huu kwa njia ya mtandao
Katika kitabu cha Yakobo 4:3 tunasoma "Mwaomba wala hampati .........." Imetokea kwamba mwanadamu ana maswali mengi saaana anayojiuliza hasa anapopita katika kipindi cha matatizo au majaribu. Ni vema kutambua kuwa tatizo si jaribu. Tatizo linakuwa jaribu pale linapokufikisha njia panda. Unapofika mahali ambapo huna msaada mwingine wa kukusaidia ktk sehemu uliyopo unaanza kutengeneza mawazo na hayo mawazo yanakupeleke kwenye kitu kinaitwa jaribu. Katika vipindi hivi mwanadamu amekuwa akiishi maisha yenye nidhamu ya uwoga. Someone define worry as a trickle of fear that meander through the mind and cut down the channel on which all other thought flow. Uwoga ulionao ni kwa sababu umejitwika mzigo usio wako. Wapo waswahili wasemao kamwe Mgomba hauwezi kushindwa na mkungu. Wapo wanaofikiri majaribu wanayopitia ni makubwa kuliko uhimili wao. Mungu hawezi kukuruhusu wewe kuingia kwenye jaribu ambalo si saizi yako. Hata hivyo umesahau kuwa jukumu ya jaribu lako halipo kwako lipo kwa YESU KRISTO wa Nazarethi aliyeubeba msalaba kwa ajili yako. Usiwe mwoga kama wale walioleta taarifa kwa Musa wakisema nchi ile ina majitu makubwa nasi tumeogopa tukajiona kama panzi. ondoa roho ya uwoga.
Haya sasa ngoja nikueleze kwa nini maombi yako yamekuwa hayajibiwi. Watu wengi wanapokuwa ktk majaribu wanauliza maswali vibaya mfano kwa jinsi gani nitatoka hapa?, kwa nini mimi tu? kweli MUNGU umeniacha?nk Haya maombi hayawezi kuwa na majibu. Badala yake jiulize Ni kwa jinsi gani nitampa MUNGU utukufu katika jaribu hili. Hili ni swali moja tuu lakini majibu yake yatakuja kama mvua ya mwanga ulioletwa katika uwanja ulio na giza. Hana aliomba mtoto kwa Mungu ili akamringishie mwenzake Sara na hakupata Alipokutana na Kuhani ELI akamfundisha namna ya kuomba. akaomba Mungu nipe mtoto Atakuwa mtumishi wako. Mwaka ule ule akampata Samweli. Jiulize maswali yatakayokupa majibu mapema AMEEEEN.
Aaamen, Asante sana Mtumishi wa Mungu, BWANA na alibariki Neno lake.
ReplyDelete