GOMBO LA WIKI
Na: Samwel Mkumbo
Sehemu ya 2.
“HUZUNI YA JINSI YA MUNGU”
Katika
wiki hii tunaendelea na mtiririko wa kujifunza somo linaloitwa “HUZUNI YA JINSI
YA MUNGU”, na wiki iliyopita tulijifunza mambo kadhaa, na mstari wetu mkuu
tunaoutumia katika Somo hili ni ule wa
2 Wakorintho 7:10 na katika
huo tutajifunza mengi zaidi……..
KARIBU!!
2 Wakorintho 7:10, umeandikwa hivi;
“Maana huzuni iliyo kwa jinsi ya
Mungu hufanya toba liletalo wokovu lisilo na majuto; bali huzuni ya dunia
hufanya mauti.”
Kujutia dhambi.
Ili
mtu aweze kujutia dhambi ni lazima kuwepo na mguso wa ndani ya moyo (nafsi
yake), lakini hii si hatua ya mwisho, maana wengi wanapotoka hatua ya kwanza
(Kutambua Kosa) huwa wanaishia kwenye hii hatua ya pili ya “Kujutia” lile
alilolitambua kuwa ni kosa ndani yake na huwa wanaishia hapo,
Luka
15:17 utakuta maneno haya:-
Alipozingatia
moyo mwake alisema ……………….. “mwana mpotevu hakuwa na cha kufanya
baada ya kutambua dhambu yake ila kwanza kujutia moyoni”. NA HATUWEZI KUJUTIA
DHAMBI BILA YAKUITAMBUA DHAMBI. Sasa
baada ya hatua hii ya kujutia dhambi ambayo inatokana na Kutambua Dhambi kuna
hatua nyingine zaidi zinazofuata mbele baada ya hapo.
Kabla
sijaendelea jikumbushe tulipoanzia na pia utambue kuwa tunajifunza kuhusu
“HUZUNI YA JINSI YA MUNGU”.
Kukiri
dhambi.
Ni
hali kuwa kukubali kuwa lile ulilofanya ni dhambi/kosa na kuwa wazi ya kuwa
nawe watambua kuwa ni kosa, kuna shida kwa watu wengi sana ya kutokubali
kukosea na kama wamekosea huwa na mawazo ya kila namna ya kufanya lile
walilotenda kuwa si kosa na hivyo HUJARIBU KUJITETEA, na katika kujitete huko
ndiko huleta makosa zaidi.
Kielelezo:
Habari za Adamu kumkosea MUNGU na namna alivyotafuta kujitetea, tukisoma katika
kitabu cha Mwanzo 3:11-12 inasema
hivi;
11Akasema,
Ni nani aliyekuambia ya kuwa u uchi? Je! Umekula wewe matunda ya mti
niliyokuagiza usiyale? 12 Adamu akasema, Huyo mwanamke uliyenipa awe
pamoja nami ndiye aliyenipa matunda ya mti huo, nikala.
Katika
mistari hiyo hapo juu utagundua namna mtu anayejaribu kukwepa kukiri kosa
alilolifanya kunavyoweza kuleta madhara, maana swali alilouliza MUNGU na jibu
alilojibu Adamu ni tofauti lakini hii inatokana na kutokuwa na moyo wa kukiri
kosa,. Tazama nami hivi;
…….. Je! Umekula wewe matunda ya mti
niliyokuagiza usiyale? Hili lilikuwa ni swali la Mungu kwa Adamu kutokana
na kuambiwa kwamba yu uchi.
………Adamu akasema, HUYO MWANAMKE
ULIYENIPA awe pamoja nami ndiye aliyenipa matunda… hili ndilo lilikuwa ni jibu la Adamu
baada ya kuulizwa na MUNGU kama amekula matunda ya mti aliyokatazwa asile.
Tazama
nami: Baada ya Adamu kula tunda alilokatazwa asile papo hapo ALITAMBUA
KOSA/DHAMBI aliyokuwa amefanya na moyoni mwake akaanza kujutia kile lichokuwa
amefanya.
Na hili linaonekana katika Mwanzo 3:7 inasema hivi;
“Wakafumbuliwa macho wote wawili
wakajijua kuwa wa uchi, wakashona majani ya mtini, wakajifanyia nguo.” Ukitazama hapo utaona neno
WAKAFUMBULIWA MACHO WOTE WAWILI…… ikiwa na maana baada tu ya kula tunda
“Wakatambua ya kuwa wamekosea” maana waliona matokeo ya kile walichokifanya
papo hapo na ndio maana wakajificha machoni pa Mungu.
Hivyo
basi Adamu ndani yake alikuwa ameshavuka hatua ya kwanza ya KUTAMBUA
KOSA/DHAMBI, lakini pia katika hatua hiyo tunaona na suala lingine ya kwamba
Adamu ALIJUTIA KOSA/DHAMBIA aliyofanya na ndio maana tunaona suala la
Mahangaiko linatokea, kwa maana ilibidi waanze kutafuta namna ya” Kujisitiri
Utupu wao” maandiko yananena “…..wakashona
majani ya mtini, wakajifanyia nguo.”
Labda
nikujulishe hili japo nitakueleza kwa undani zaidi huko mbele tunapoendelea
kujifunza ya kwamba Hatua ya KUJUTIA KOSA/DHAMBI huja na maangaiko ya ndani na
nje. Na ndio maana ule mstari wa 2Wakorintho
7:10 kuna maneno yanayosema bali
huzuni ya dunia hufanya mauti.”, lakini pia nikuongezee maarifa kwa kukueleza
ya kwamba moja ya jambo lililo karibu na Mahangaiko ni “Mauti” hivyo inapotokea mtu akatenda kosa halafu ndani yake
ikaingia roho ya mahangaiko inayotokana na Kutambua na Kujutia Kosa
kunahitajika Nguvu ya Mungu inayokuja kwa njia ya Huzuni ili kumfanya AKIRI
KOSA NA KUTUBU.
Nitakuambia
kwa kirefu baadae, lakini ni hivi; kwa hali ya kawaida mwanadamu mwenyewe ni
kazi kujipeleka katika hatua ya KUKIRI NA KUTUBU KOSA/DHAMBI bali huwa anaishia
katika hatua ya KUTAMBUA NA KUJUTIA, na tatizo kubwa ni kwamba kama mtu
anaishia kwenye kujuta tu basi yale majuto yasipokutana na “HUZUNI YA JINSI YA
MUNGU” ambayo inapelekea mtu Kukiri na
Kutubu basi mauti huwa inachukua nafasi.
Zaburi 32:5b tunasoma:-
Nalisema nitayakiri maovu yangu kwa
BWANA,
Nawe ukanisamehe upotevu wa dhambi
yangu.
Tazama
nami:
Kukiri dhambi huwa nje ya mtu na hutokana na
kujutia dhambi kunakofanyika ndani ya mtu.
2 samweli 12:13 tunakuta nmaneno haya;
“Daudi akamwambia Nathani,
Nimemfanyia Bwana dhambi……………….. mfalme
Daudi alipotambua kosa alilolifanya na kulijutia ndani yake alikiri mbele ya
nabii nathani ya kuwa Amemfanyia Bwana dhambi. Hakukaa kimya wala hakutaka
kumsingia mkewe Huria kuwa alikuwa amesababisha kwa kosa la kuoga nje mchana.
Naam! Angeweza tu kurudisha kosa kwa mkewe Huria kama alivyofanya Adamu kwa
kusema “Ni huyu mwanamke uliyenipa….” Maana anataka kumtuhumu Mungu kwamba
asingempa huyo mwanamke basi asingekula tunda.
Lakini
Daudi yeye alikiri kabisa ya kwamba amemfanyia Mungu dhambi na alikubali na hiyo
inatokana na matokeo ya kujutia dhambi kulikotokea ndani ya Daudi. Na hii ni
kwa sababu “HUZUNI YA JINSI YA MUNGU” iliingia ndani ya Daudi ambayo inamtoa
kwenye Hatua ya Kutambua Kosan a Kujutia na hiyo huzuni inampeleka kwenye
KUKIRI hilo kosa pia.
Itaendelea………………………………………………….
No comments:
Post a Comment