GOMBO LA WIKI
Na: Samwel Mkumbo
Sehemu
ya 3.
“HUZUNI YA JINSI YA MUNGU”
Katika
wiki hii tunaendelea na mtiririko wa kujifunza somo linaloitwa “HUZUNI YA JINSI
YA MUNGU”, na wiki iliyopita tulijifunza mambo kadhaa, na mstari wetu mkuu
tunaoutumia katika Somo hili ni ule wa
2 Wakorintho 7:10 na katika
huo tutajifunza mengi zaidi……..
KARIBU!!
2 Wakorintho 7:10, umeandikwa hivi;
“Maana huzuni iliyo kwa jinsi ya
Mungu hufanya toba liletalo wokovu lisilo na majuto; bali huzuni ya dunia
hufanya mauti.”
Wiki
iliyopita katika sehemu ya pili tulitazama suala la KUKIRI DHAMBI, na naamini
kwa jinsi tulivyolitazama kwa undani utakuwa umepata jambo la kukusaidia. Sasa baada
ya hatua tulizokwisha kuzitazama. Tuendelee, na kumbuka haya ninayokufundisha
ndiyo yatakayokuja kutusaidia nitakapokuwa nakuonesha TOFAUTI YA HUZUNI YA
JINSI YA MUNGU, na ile HUZUNI YA DUNIA.
Kutubu
dhambi.
Kwa
maneno rahisi ni kuamua/ kukata shauri kwa kuamua kubadili njia ambayo ulikuwa
unapita katika maisha yako au jambo Fulani maishani mwako, nah ii inatokana na
njia au hatua nilizokuelezea nyuma kupita.
Yaani
ili mtu afikie hatua hii ya Kutubu dhambi au kosa ni lazima kwanza awe
AMELITAMBUA KOSA/DHAMBI yenyewe, kisha KUJUTUTIA halafu tena KUKIRI ndiposa
KUTUBU HUFUATA.
Lakini
zaidi ya hayo niliyokwisha kukueleza hapo juu, natamani nikuongezee jambo ya
kwamba kwa ujumla wake wa hayo niliyokufundisha katika sehemu mbili zilizopita,
ni kwamba KUTUBU huja kutokana na KUKUBALI NA KUTII.
Hayo
ndiyo maelezo mafupi yanayoweza kumeza mambo mengi niliyokuandikia hapo juu, ni
kwamba KUTUBU ni matokeo ya KUKUBALI na KUTII. Na labda ngoja nikueleze maana
ya Kukubali na Kutii.
Kukubali
Maana
ya haraka ya neno “Kukubali” Ni kuwa tayari kufundishwa na BWANA ili upate
ufahamu. hii inanipa uwezo wa kukwambia kuwa jambo la msingi ili upate
kufundishwa na upate ufahamu ni kuwa tayari kufundishwa na huyo anayekufundisha
huko ndiko kunaitwa kukubali na ndiko kunaleta mabadiliko ya ndani na ya nje
kwa mtu yeyote Yule.
Isaya 48:16-17 inasema hivi;
“16Nikaribieni,
sikieni haya; tokea mwanzo sikunena kwa siri; tangu yalipokuwapo, mimi nipo; na
sasa Bwana MUNGU amenituma, na roho yake.17 Bwana, mkombozi wako,
mtakatifu wa Israeli, asema hivi; Mimi ni Bwana, Mungu wako, nikufundishaye ili
upate faida, nikuongozaye kwa njia ikupasayo kuifuata.
Sasa
nataka nikuoneshe maneno haya;..,……. 16 Nikaribieni, sikieni haya;…… Mimi ni Bwana, Mungu wako,
nikufundishaye…………. Mungu anaanza na neno NIKARIBIENI, maana yake ni wito
anaokuita, kabla Mungu hajakufundisha kwanza anakuita mana hawezi kukufundisha
ukiwa umezagaa zagaa tu au uko mbali nae, au uko katika hali ya kuhangaika.
Huwa kwanza anakuita anasema NIKARIBIE, kisha anaongeza neno la msingi ambalo
linaashiria “Utulivu”, pale anaposema SIKIENI HAYA… anachotaka kwanza ni
utulivu wa mtu. Sasa mtu Yule anayetenda yote haya, yaani ANAEKARIBIA (kusikia
wito/mwaliko) halafu ASIKIE HAYA….(anayetulia) ndiye anayepata nafasi ya
KUFUNDISHWA NA BWANA, na huko ndiko tunaita KUKUBALI.
Baada
ya kukueleza hilo, nataka nikutazamishe jambo kidogo ili ujue zaidi juu ya
kufundisha na BWANA.
Zaburi 32:8 tunakuta maneno haya; “Nitakufundisha na kukuonyesha njia
utakayoiendea;……..” sasa kwa hali ya kawaida neno kufundisha lina maana ya
“Kupewa Maelekezo juu ya jambo Fulani”. Hivyo Mungu anaposema “Nitakufundisha”
maana yake “Nitakupa maelekezo”. Sasa basi ikiwa nimekwambia KUTUBU ni matokeo
ya Kukubali na Kutii ina maana Kutubu ni matokeo ya Kuwa tayari
kufundishwa/Kupewa maelekezo na Kutii., (nitakuambia maana ya kutii mbele
kidogo). Basi kwa maelezo mafupi tunaweza kusema mtu anapofikia hatua ya Kutubu
ni lazima hapo nyuma “Alikubali kufundishwa/kupewa maelekezo na Akatii hayo”.
Mtu
anapofundishwa itamwezesha kufanya au kutokufanya hatua inayofuata yaani Kutii.
Kutii
Ni
kufanya kile ulichoamriwa baada ya kufundishwa, yaani baada ya kukubali
kufundishwa ambapo nilikwambia ni Kupewa maelekezo, sasa ile hali ya kufanya
jambo kama umepewa maelekezo ya kufanya au kutofanya jambo kama umepewa
maelekezo ya kutofanya ndio inayoitwa Kutii.
Luka
5:5 inasema
hivi;
Simoni
akajibu akamwambia, Bwana mkubwa, tumefanya kazi ya kuchosha usiku kucha,
tusipate kitu; lakini kwa neno lako nitazishusha nyavu.
Kauli
anayosema Simoni inaweza kutupa mtazamo halisi wa hili ninalokufundisha hapa,
tazama maneno haya “……… lakini kwa neno lako nitazishusha nyavu.
Simoni
anachoonesha ni kwamba kitendo chake cha kushusha nyavu ni matokeo ya maelekezo
aliyoyapata kutoka katika “NENO LILILOSEMWA NA YESU”, ahaa, hivyo basi Yesu
angemwambia “asishushe nyavu” ni kweli asingeshusha maana kwa wakati huo
alikuwa anategemea Neno toka kwa Yesu ili Atii.
Yohana 5:8-9 inasema;
Yesu akamwambia, Simama, jitwike
godoro lako, uende. 9 Mara yule mtu akawa mzima, akajitwika godoro
lake, akaenda…………….
Sasa
labda nikupe maelezo ya kina hapa katika habari ya Kutii, mara nyingi kutii
hutokea wakati mtu anapoambiwa aua anapopewa maelekezo ya kufanya jambo ambalo
kwa akili ya kawaida(kibinadamu) au ufahamu wake inakuwa kama haiwezi kuwa. Na
ndio maana huyo mtu (katika Yohana 5:8-9) kama ukianzia kusoma tangu mistari ya
mwanzoni ni mtu aliugua kwa miaka mingi, na hakuweza kupona na imani ya kupona
kwake aliiweka kwenye maji ya birika. Lakini Yesu alipokuja aliibadilisha na
hivyo huyu mtu alihitajika kuwa na Utii.
Ahaa,
sasa basi hii tunaweza kuileta hata katika habari ya “kutubu” Kutii
kunahitajika maana unaweza kupewa maelekezo kwa kufundishwa yanayokutaka uache
au usitende jambo ambalo kwa hali ya kawaida (kibinadamu) unaweza kuliona si
Tatizo hatakidogo wala halina shida. NA HAPO NDIPOSA MUNGU HUTUMIA HUZUNI ILIYO
YA JINSI YA MUNGU ILI KUWEKA NGUVU ITAKAYOKUKIMBIZA KUTUBU.
Tazama
nami:
“Huzuni ya Jinsi ya Mungu” ni
matokeo ya Kutambua, Kujutia na Kukiri Kosa lakini ili ikamilike zaidi Huzuni
ya Jinsi ya Mungu hukupeleka “Kutubu” maana katikati ya Huzuni ya Jinsi ya
Mungu kuna maelekezo (mafundisho) yanayokuja yatakayokuhitaji uyatende na
unapoyatenda ndio kutii na hayo maelekezo hayatakupelekea mahali pengine kama
ni suala linalohusu Dhambi/Kosa zaidi ya kukutaka “Utubu”.
Na
hiyo ndiyo tofauti kubwa nitakayokueleza hapo mbele, kati ya “Huzuni ya Jinsi
ya Mungu” na ile ya Dunia.
Tazama
nami tena:
Huzuni
ya Dunia haiwezi kukupeleka mwisho mzuri, haiwezi kukufanya uangalie kuwa kuna
tumaini tena pale unapokuwa katika hali ngumu na ya dhiki, ndio! Huzuni ya
Dunia haiwezi kukufanya utazame kuwa kuna Mungu, ila inakufanya Uone kuna MUNGU
aliyejiandaa kuhukumu tu na wala si kusamehe. Huzuni ya Dunia inakufanya uone
ulilolifanya limekuangamiza wala hakuna njia tena, wala hakuna kutoka tena,
kama ni hali ya umasikini, huzuni ya dunia itakuambia ulipokataa kutoa rushwa
ili upate kazi ulikosea, kama ni binti itakuambia kutovaa mavazi yanayoonyesha
mwili wako ndio kumekufanya usiolewe hata leo, kama ni magonjwa huzuni ya dunia
itakwambia ulipokataa kwenda kwa mganga ndio umejiangamiza, ujumla wa yote hayo
ni MAJUTO na majuto HULETA MAUTI …… bali
huzuni ya dunia hufanya mauti.” (2 Wakorintho 7:10) HIYO NDIO HUZUNI YA
DUNIA,
ITAENDELEA………… DOWNLOAD HERE
No comments:
Post a Comment