Tazama nami:
“Kuna Uhusiano Mkubwa kati ya Usalama
na Ubora wa Nafsi yako na Uhai wa Kanisa”
Na:
Mwl. Samwel Mkumbo
USALAMA NA UBORA WA NAFSI YAKO UNAVYOHUSIANA NA UHAI WA KANISA
Sehemu ya 3.
Utangulizi:
Katika mifululizo yote ya somo hili kutoka mwanzo
mpaka sasa imekuwa ni suala la
kuangalia ni kwa jinsi gani
nafsi zetu zinahusika sana katika Uhai wa Kanisa. Sehemu ya
mwisho nitasema nawe kwa
kifupi sana kuhusu Uhusiano wa nafsi ya Kanisa.
Karibu tujifunze pamoja…..
Luka
12:15 inasema hivi;
Akawaambia,
Angalieni, jilindeni na choyo, maana uzima wa mtu haumo katika wingi wa vitu
vyake alivyo navyo.
Ni heri kila mmoja
akahakikisha ya kwamba Nafsi yake iko na furaha kila wakati, kwa ajili ya uhai
wa kanisa lako, lakini pia kwa ajili ya uhai wa nyumba yako kama msingi wa
kanisa, kwa ajili ya ofisi yako, kwa ajili ya ukoo wako.
Lakini pia ni vema kila
mmoja akahakikisha anafanya bidii kumfurahisha mwingine na kuifanya nafsi ya
mwingine isiwe na jeraha hata moja, kuifanya nafsi ya mwingine isitende dhambi,
kila mmoja acheze karibu na mwenzake, kama kucheza basi tucheze peke yetu,
hakikisha unamlinda mwenzake asipate shida wala asipotee.
1
Wakorintho 8:12 tunasoma hivi;
Hivyo,
mkiwatenda dhambi ndugu zenu na kuitia jeraha dhamiri iliyo dhaifu, mnamtenda
dhambi Kristo
Kuna
Uhusiano Mkubwa kati ya Usalama na
Ubora
wa Nafsi yako na Uhai wa Kanisa
Sasa labda tutazame kwa nafasi nyingine uhusiano wa Nafsi
yako ikiwa na Usalama na ubora wa nafsi yako na Uhai wa Kanisa ikiwa ni la
nyumbani au ni mahali unapoabudu au ofisini kwako au hata shuleni kwako
unakosoma.
Labda niweke jambo hili la msingi, tunapozungumzia kanisa
ni lazima tukajua ya kwamba si suala la dhehebu moja tu au suala la watu
wanaosali kwa pamoja lakini suala la Kanisa ni jambo linalohusu watu wote
waliookoka na wanaomkubali BWANA YESU kuwa ni mwokozi wa maisha yao na Mfalme
wa Ulimwengu wote.
Sasa kuna shida ambayo ni muhimu tukaishughulikia vizuri
kidogo ili tusipate shida tunapoangalia utekelezaji wa Somo hili, na jambo
lenyewe ni lazima akili zetu na fahamu zetu zifunguke tukajua mambo kadhaa ili
tuone Umuhimu wa kuona Nafsi ya kila mmoja inakuwa salama na bora ili Kanisa
liweze kuwa Hai.
1
Wakorintho 3:16-17 tunasoma hivi;
Hamjui
ya kuwa ninyi mmekuwa hekalu la Mungu, na ya kuwa Roho wa Mungu anakaa ndani
yenu? Kama mtu akiliharibu hekalu la Mungu, Mungu atamharibu mtu huyo. Kwa
maana hekalu la Mungu ni takatifu, ambalo ndilo ninyi.
Sasa kuna jambo la msingi hapo natamani tulitazame kwa
makini sana sana, maana kama tusipolitazama kwa makini tunaweza tusielewe
vizuri, na hilo jambo linatuonesha Uhusiano uliopo kati ya Usalama na Ubora wa
Nafsi yako inavyohusiana na Uhai wa Kanisa la Tanzania, Kanisa la Ulimwengu
mzima lakini pia kuanzia na Kanisa la Nyumbani kwako na mahali unapoabudu.
Basi tuutazame huo mstari kwa makini sana sana, kuna
maneno kadhaa ya huo mstari natamani tuyatazame kwa makini …..Hamjui ya kuwa NINYI mmekuwa hekalu la
Mungu….. na ya kuwa Roho wa Mungu anakaa ndani YENU?....... Kama MTU
akiliharibu hekalu la Mungu,… Mungu atamharibu MTU huyo….. Kwa maana hekalu la
Mungu ni takatifu, ambalo ndilo NINYI.
Maneno niliyoyaweka kwa herufi kubwa yana maana kubwa
sana, Paulo kwa uwezo wa Roho Mtakatifu anawaandikia Wakorintho akitaka
kuwaonesha ni jinsi gani Uhusiano wa Kanisa unavyotengenezwa na unavyotegemea
mtu mmoja mmoja. Anapozungumzia Hekalu la Mungu anasema ni NINYI au ndilo SISI
kama tukijiweka kwenye nafasi ya Wakorintho na ambayo ni nafasi muhimu lazima
tujiweke hapo ili hiyo nafasi tuichukue kwa Umuhimu mkubwa sana.
Jambo amabalo ni la kulitazama kwa makini kwenye mistari
hiyo ni kwamba inapozungumziwa kanisa basi tunatazama kama Muunganiko wa watu,.
Maana HEKALU LA MUNGU (moja) linajengwa na NINYI (wengi), lakini pia
inawezekana hilo Hekalu la Mungu ambalo ni watu wengi likaharibiwa na MTU yaani
mmoja. Sasa basi kuna jambo la kulitazama tena hapo kwa makini Zaidi, kwamba
kama Hekalu la Mungu linalojengwa na SISI linaweza kuharibu na YULE au WEWE
basi pia linaweza kujengwa na WEWE- Nitalielezea hilo baadae kwa undani.
1Wakorintho
6:19
tunasoma hivi;
Au
hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu,
mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe;
Nataka tutazame vizuri maneno mengine kwenye mstari huo
ambayo hayatofautiani sana maneno yaliyoelezwa kwenye mistari ile
tuliyotangulia kuitazama hapo juu (1Wakorintho 3:16-17), maana katika mstari
huo hapo anaeleza wingi wa waliookoka kama mtu mmoja na ambaye huyo mtu mmoja
anatengeneza Hekalu la Mungu, lakini cha ajabu Paulo anaandika kwa wengi kana
kwamba kwa mtu mmoja.
Tazama kwa makini maneno haya;
Au
HAMJUI ya kuwa MWILI WENU ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani YENU,
MLIYEPEWA na Mungu? Wala NINYI si mali YENU wenyewe;
Anasema hivi
Au
HAMJUI (wengi) ya kuwa
MWILI WENU (mmoja) ni hekalu la Roho
Mtakatifu aliye ndani YENU MLIYEPEWA (wengi) na Mungu? Wala NINYI si mali YENU wenyewe;
Katika yote nataka nikuoneshe ya kwamba haijalishi kwa
Ukubwa wake au kwa udogo wake, kwa umaarufu wake au kwa kutokujulikana kwake,
KANISA linaanza na Nafsi moja moja na haijalishi kwa wingi wake waliopo humo
ndaniau idadi ya waliookoka katika mji Fulani au nchi Fulani bado kanisa
litahesabika kama MTU MMOJA au MWILI MMOJA.
Mpaka hapo tujaribu kurudi kidogo kwenye ule mstari wa 1Wakorintho 3:17 unasema hivi;
Kama
mtu akiliharibu hekalu la Mungu, Mungu atamharibu mtu huyo. Kwa maana hekalu la
Mungu ni takatifu, ambalo ndilo ninyi.
Nataka tuone madhara yanayoweza kutokea mtu anapojaribu
kuliharibu Hekalu la Mungu yaani Kanisa ambalo ni Ninyi mlio wengi
mnaotengeneza Mtu au Kitu kimoja katika kumtukuza Kristo au kusimamisha Ufalme
wa Mungu. Maandiko yanasema mtu akiliharibu Hekalu MUNGU atamharibu mtu huyo.
Sasa tuondoe mawazo ya kuwafikiria watu kama wakina Sauli
ambao wanaliharibu Hekalu au Kanisa kwa sababu Hawajaokoka, au tusiwafikirie
Wakuu wa makuhani wanaokataza watu wasiseme tena wala kupoza Wagonjwa kwa Jina
la YESU, tukiangalia hivyo tutakosa maana ya msingi sana sana, hebu tuutazame
huo mstari kama unawaambia watu au unamuonya Mtu anayeliharibu Kanisa huku naye
ameokoka au yumo ndani ya Kanisa.
Na kulingana na maandiko inawezekana kabisa mtu
akaliharibu Kanisa wakati mwenyewe yumo humo ndani yake, haijalishi anajua kama
analiharibu Kanisa au la, lakini kuna uwezekano kabisa akawa analiharibu kanisa
wakati na yeye yumo ndani yake.
Matendo
20:28-30 tunasoma hivi;
Jitunzeni
nafsi zenu, na lile kundi lote nalo, ambalo Roho Mtakatifu amewaweka ninyi kuwa
waangalizi ndani yake, mpate kulilisha kanisa lake Mungu, alilolinunua kwa damu
yake mwenyewe. Najua mimi ya kuwa baada ya kuondoka kwangu mbwa-mwitu wakali
wataingia kwenu, wasilihurumie kundi; tena katika ninyi wenyewe watainuka watu
wakisema mapotovu, wawavute hao wanafunzi wawaandamie wao.
Sasa kuanzia mstari wa 30 inaonesha kabisa ya kwamba si
kwamba mharibu anaweza kutoka nje ya kundi lakini kumbe anaweza kutoka ndani ya
kundi, hata kama ataonekana ni kama mtu anayekata tawi alilokalia mwenyewe
lakini hiyo si kitu lakini ndio anaharibu sasa. Na MUNGU hawezi kukaa kimya
anapomuona mtu anaharibu au anapoleta au kuingiza kitu kinachoharibu kanisa
hata kama huyo mtu hajui lakini MUNGU hatamuacha, lazima atampa adhabu
Kulingana na ule mstari wa 1Wakorintho 3:17.
Lakini nataka niweke jambo Fulani ndani yako ya kwamba,
kama mtu alikuwa mpo naye pamoja kasha akaanza kutenda mambo tofauti na
kuliharibu kundi lazima mtapata shida, lakini pia MUNGU akimhadhibu mtu huyo
bado kwa watu wenye Uchungu na Kanisa watapata shida lazima maana wanajua
Umuhimu wake, hivyo hawatafurahia adhabu ya MUNGU aliyoipata, hivyo basi Nafsi
moja ikiharibika lazima kuna jambo linabadilika kwenye Kanisa.
Matendo
5:5-11 inasema hivi;
Anania
aliposikia maneno haya akaanguka, akafa. Hofu nyingi ikawapata watu wote
walioyasikia haya. Vijana wakaondoka, wakamtia katika sanda, wakamchukua nje,
wakamzika. Hata muda wa saa tatu baadaye mkewe akaingia, naye hana habari ya
hayo yaliyotokea. Petro akamjibu, Niambie, Mlikiuza kiwanja kwa thamani hiyo?
Akasema, Ndiyo, kwa thamani hiyo. Petro akamwambia, Imekuwaje hata mkapatana
kumjaribu Roho wa Bwana? Angalia, miguu yao waliomzika mumeo ipo mlangoni, nao
watakuchukua nje wewe nawe. Mara akaanguka miguuni pake akafa; wale vijana
wakaingia wakamkuta amekufa, wakamchukua nje, wakamzika pamoja na mumewe. Hofu
nyingi ikawapata kanisa lote na watu wote walioyasikia haya.
katika mistari hiyo natamani nikuoneshe kilichotokea kwa
Anania na Safira na Uhusiano na Kanisa, sasa ninawinda mstari ule wa 11 ambao
unatuonesha jambo Fulani lililotokea kwenye Kanisa na jambo lenyewe ni HOFU
iliyo ZIMISHA nafsi zao kwa ndani, sio hofu tu ya kusema MUNGU ni MKUU lakini
pia inakuwaje mtu akiwa na shida ya kuonana na Petro au mtume Fulani, na ndio
maana hawakuwa na Ujasiri wa kusema jambo lolote na waliona ni heri kutenda
dhambi ya kunung’unikakuliko kuonana na Mitume na kuwaambia shida zao.
Yote hiyo inatokana na nafsi ya mtu mmoja Anania
ilipoharibika ilikuwa haiku Salama iliyomshauri Mkewe Safira na wote wakatenda
jambo lililoharibu Kanisa kwa namna moja au nyingine, na halikuharibu kanisa
kwa mtindo ambao watu waliondoka, la hasha! Watu walikuwepo na walizidi
kuongezeka katika kanisa (MATENDO 4:14)
lakini ndani yake kuna WOGA/HOFU ambayo ilisababisha watu wawaogope mitume
kuwaeleza shida zao wakaona ni vema tu wakanung’unika (MATENDO 6:1)
Nataka niseme ya kwamba suala si tu kuona watu, lakini
Nafsi ya kila mmoja inatakiwa iwe Salama, maana nafsi Fulani ikiharibika basi
ujue hakuna Usalama hapo, na ujue kabisa kunahitajika kuhakikisha kila nafsi
ndani ya Kanisa iko Salama na iko Bora.
Waebrania
12:15 tunasoma;
Mkiangalia
sana mtu asiipungukie neema ya Mungu; shina la uchungu lisije likachipuka na
kuwasumbua, na watu wengi wakatiwa unajisi kwa hilo.
Nimeweka huo mstari hapo ili
tutazame jambo hilo kwa mtazamo wa Upande wa pili ya kwamba kama mtu mmoja
akipungukiwa na Neema ya Mungu anaweza kuleta shina la Uchungu ambalo
linawakwaza wengi, Je ikatokea mtu mmoja akaongezewa Neema ya Mungu nini
kitatokea? Nadhani shina jema shina la utamu, shina la furaha, shina la
kicheko, shina la wema linachipuka na KUWABARIKI WENGI.
DOWNLOAD HERE
No comments:
Post a Comment